Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama anawatangazia wananchi wote wa Butiama kujitokeza katika vitongoji vyao kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki kwenye zoezi la uchanguzi wa Serikali za mitaa unaotegemea kufanyika mnamo tarehe 24 Novemba ,2019.
Zoezi hilo la Uandikishaji litafanyika kwa kila kitongoji kuanzia tarehe 08 Novemba,2019 hadi tarehe 14/Novemba ,2019 .Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni
Kumbuka :Vitambulisho vya kupigia kura vilivyotolewa na tume ya uchaguzi havitahusika katika uchaguzi bali vitahusika katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.Hivyo kama mtu hatajiandikisha kwenye daftari la serikali za mitaa Hatashiriki kupiga kura kumchagua Mwenyekiti wake wa Kitongoji,Kijiji na wajumbe wa serikali ya kijiji
Butiama District Council
Anuani ya posta: P.O.BOX 1207 BUTIAMA
Simu: (028)2623121
Simu: 0767300061/756357458
Barua pepe: ded@butiamadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Butiama.Haki zote zimehifadhiwa