Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ilianzishwa mwezi Agosti 2013, kabla ya hapo ilikuwa ni sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma vijijini. Halmashauri hii ndipo alipozaliwa baba waTaifa la Tanzania hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere.
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ina jumla ya eneo la kilometa za mraba 2,257.127. Kati ya eneo hilo kilometa za mraba 103 limefunikwa na ziwa Victoria.
Butiama kama yalivyo maeneo mengine ya kanda yaziwa hasa katika mkoa wa Mara ina misimu miwili tu ya mvua, kwa maana ya mvua za vuli ambazo hunyesha kati ya mwezi wa Oktoba hadi Desemba, na msimu mwingine wa mvua ni mvua za masika ambazo hunyesha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei.
Halmashauri ya Wilayaya Butiama ina nyuzi joto za sentigredi kati ya 24 na 32.
Wakazi wa Halmashauri hii wanajihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji, biashara, uvuvi pamoja na uchimbaji wa madini.
Mazao ya kilimo yanayopatikana Butiama ni mahindi, viazi mviringo, viazi vitamu n.k.
MUUNDO WA UTAWALA BUTIAMA
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama inajumla ya tarafa mbili (2), kata kumi na nane(18), vijiji hamsini na tisa(59) na vitongoji mia tatu na sabini (370). Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndiye kiongozi mkuu wa taasisi akisaidiwa na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri kwa maana ya wakuu wa Idara na vitengo.
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ina jumla ya Idara kumi na mbili na vitengo sita. Idara hizo ni hizi zifuatazo; Idara ya Utumishi na Utawala, Idara ya Mipango, takwimu na ufuatiliaji, Idara ya Afya, Idara ya Fedha na biashara, Idara ya Elimu msingi, Idara ya Elimu sekondari, Idara ya Kilimo ushirika na umwagiliaji, Idara ya Mifugo na uvuvi, Idara ya Ardhi na mal iasili, Idara ya Maendeleo ya jamii, Idara ya ujenzi na Idara ya Maji.
Pamoja na Idara hizo Halmashauri ya Butiama ina vitengo vifuatavyo; Kitengo cha sheria, Kitengo cha ukaguzi wa ndani, Kitengo cha Teknolojia ya habari na mawasiliano, Kitengo cha ugavi,Kitengo cha uchaguzi na Kitengo cha ufugaji nyuki.
Butiama District Council
Anuani ya posta: P.O.BOX 1207 BUTIAMA
Simu: (028)2623121
Simu: 0767300061/756357458
Barua pepe: ded@butiamadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Butiama.Haki zote zimehifadhiwa