Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Gosbert B.Rwakeza amefungua Mafunzo kwa kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Kata na kuwataka Kuonesha Uaminifu na Utiifu wa kusimamia Sheria na taratibu za utoaji wa Mikopo kwa ngazi yao ili kuitimiza azma ya Serikali kutoa Mikopo hiyo kwa Vikundi vya Wanawake,Vijana na wenye Ulemavu.
Kaimu Mkurugenzi amesema,Serikali imeamua Kuleta Mfumo na Muongozo Mpya wa utoaji wa Mikopo ili kuepusha udanganyifu na kulinda fedha hizo na Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakaekaidi.
Halmashauri ya wilaya ya Butiaama imetenga zaidi ya shilingi milioni 350 kukopesha Vikundi vya Wanawake Vijana na Wenye Ulemavu.
Aidha uibuaji wa vikundi hivyo utafanyika kwenye Mikutano ngazi ya kata.
Butiama District Council
Anuani ya posta: P.O.BOX 1207 BUTIAMA
Simu: (028)2623121
Simu: 0767300061/756357458
Barua pepe: ded@butiamadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Butiama.Haki zote zimehifadhiwa