Friday 27th, December 2024
@Matongo
Usiku wa tarehe 20,oct 2018 kulitokea mvua kubwa iliyoandamana na Upepo mkali katika wilaya ya Butiama .Upepo huo Uliweza kuezua jengo la Dispensari ya Kijiji cha Matongo lilokuwa limejengwa kwa nguvu za wananchi.
Wakizungumuzia tukio hilo Diwani wa kata hiyo ya Buhemba Mhe.Boniphace Masero pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Magina Nyahuko ,Wamesema wananchi wa kijiji cha matongo na vijiji vingine vinavyozunguka eneo hilo wamepata hasara kubwa kutokana na janga hilo lililosababishwa na Upepo mkali.
Jengo hilo lililokuwa limejengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na halmashauri ya Wilaya ya Butiama ,lilikuwa limeezekwa kwa ukamilifu,limepigwa ripu nje na ndani pamoja na kuwekwa milango na madirisha.
Kwa ujumla wake viongozi hao waliofika mara baada ya tukio hilo wameiomba serikali pamoja na wadau wengine kujitokeza kutoa msaada wa hali na mali kwa wananchi wa kijiji cha matongo na vijiji jirani ilijengo hilo liezekwe Upya na wananchi wapate huduma waliyokusudia.
Butiama District Council
Anuani ya posta: P.O.BOX 1207 BUTIAMA
Simu: (028)2623121
Simu: 0767300061/756357458
Barua pepe: ded@butiamadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Butiama.Haki zote zimehifadhiwa